Huu ni wasifu wa ‘Nyota Inayong’aa’ (‘Akhtar-e-Tabaan’) ambayo ilichomoza huko Bihar (India), ikang’aa katika bara India yote, na ilitia nuru kwenye njia ya Waafrika wengi kuingia kwenye Uislamu wa Shia. Kupitia kalamu yake, aliwasha taa ya Ushia kuvuka mabara na bahari kuu, kutoka Indonesia, hadi Guyana, hadi Ulaya, na ng’ambo.
‘Allāmah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi alikabiliwa na matatizo mengi mazito: nchi za ugenini, lugha, tamaduni, upinzani, chuki bila sababu, siasa & zaidi. Hata hivyo, mng’ao wake ulipenya kila mahali na kushinda viunzi vyote vilivyokuwa katika njia yake ya tablīgh.
Ni matarajio kwamba, kusoma simulizi ya maisha yake ni jambo ambalo litakutia nguvu zaidi kuwa na moyo wa kuhudumuia dhamira ya Uislamu, hata kama utakutana na changamoto katika kazi hiyo.
Kitabu hiki kina matarajio ya kudhihirisha kwamba kama mtu amejiandaa akiwa na elimu ya kweli, roho ya uvumilivu na ikhlasi, Mungu atamjaalia tawfiq na atafanikiwa.